Nafasi ya Kazi

ADP Mbozi ni shirika lisilo la kiserikali linaloendesha shughuli zake Tanzania bara, kwa madhumuni ya kutoa huduma  hitajika za maendeleo ili waweze kuboresha hali zao za maisha kiuchumi na kijamii kwa kutumia rasilimali kwa njia endelevu. Makao makuu ya shirika  hili yako  mjini Vwawa mkabala na ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Mbozi.

Kutokana na utekelezaji wa shughuli zake vijijini, Shirika linatangaza nafasi ya kazi ya Fundi magari /Dereva mwenye sifa zifuatazo:

 1. Awe na elimu ya sekondari hususani kidato cha nne.
 2. Awe na cheti cha ufundi magari kutoka vyuo vinavyotambulika na serikali
 3. Awe na leseni ya udereva daraja C
 4. Awe na umri usiozidi miaka 45
 5. Awe na uzoefu wa kutengeneza magari na udereva usiopungua miaka mitatu

Kazi za fundi magari/dereva:

 1. Kufanya sevisi/matengenezo ya vipindi ya magari ya Shirika
 2. Kufanya repea za mara kwa mara za magari ya shirika
 3. Kukagua ubora na usalama wa chombo cha usafiri kila siku asubuhi kabla ya kuaza kazi
 4. Kuendesha chombo cha usafiri kwa umakini na weledi
 5. Kuweka kumbukumbu za kilometa za chombo cha usafiri kwenye kitabu cha gari ( Log book)
 6. Kutoa taarifa juu ya muda wa sevisi ya chombo cha usafiri na kusimamia /kufanya sevisi na matengenezo ya mengine
 7. Kupakia na kupakua mizigo itakayosafirishwa na chombo cha usafiri
 8. Kutoa taarifa juu ya uharibifu au ajali yoyote itakayo tokea kwa Afisa Utawala
 9. Kuweka chombo cha usafiri katika hali ya usafi wakati wote
 10. Kutunza vifaa vyote vilivyomo ndani ya chombo cha usafiri
 11. Kutekeleza majukumu mengine utakayopangiwa na kiongozi wake

Namna ya kutuma maombi:

Mwenye nia atume maombi yake kwa njia ya barua kwa Mkurugezi Mtendaji, S.L.P 204 Mbozi. Au Barua Pepe: adpmbozi @yahoo.com  Barua iambatanishwe na nakala za vyeti, Leseni na kitambulisho cha NIDA.

Mwisho wa kuwasilishwa maombi ni tarehe 18/2/2024. Tangazo hili limetolewa leo tarehe 2/2/2024